3 Februari 2017 - 19:40
 Mapigano yapamba moto Ukraine

Mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi yamesababisha vifo vya watu wawili zaidi katika mji wenye machafuko wa Avidiivka leo, na wanne wengine kwingineko,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi yamesababisha vifo vya watu wawili zaidi katika mji wenye machafuko wa Avidiivka leo, na wanne wengine kwingineko, katika umwagaji damu ulioisababisha Marekani kulaani msimamo wa Urusi ilioutaja kuwa wa uchokozi. Ripoti za karibuni kutoka pande zote mbili zimetaja idadi ya waliokufa katika mapigano tangu Jumapili kuwa watu 32, idadi ambayo haijafikiwa tangu kilele cha vita hivyo mwaka 2014 na 2015. Ukraine na Urusi zinalaumiana kuhusu nani alieanzisha vurugu hizo, na nani anahusika na vifo. Waandishi habari wa shirika la habari mjini Avdiivdka amesema leo kuwa mashambulizi yamepungua kwa kiasi kikubwa, na kwamba kinachosikika sasa ni milio ya hapa na pale ya maroketi pembezoni mwa mji huo.

Mwisho wa habari/ 291